Social Icons

Pages

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

Featured Posts

Thursday, February 1, 2018

SWAHILI LUTHERAN CHURCH INAWAKARIBISHA JUMAPILI YA TANO YA EPIPHANIA



Ban Ki-moon ashiriki ufunguzi wa Ubalozi wa Tanzania Jamhuri ya Korea


Picha ya pamoja baada ya Waziri Mahiga na Mheshimiwa Sung-nam kukata utepe na kuzindua rasmi majengo hayo. Kutoka kushoto ni Bw. Park Young min, Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Afrika; Mhe. Silvester Bile, Kiongozi wa Mabalozi wa Afrika na Balozi wa Ivory Coast; Mhe. Ban Ki-moon, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Mstaafu; Mhe. Augustine Mahiga, Waziri wa Mambo ya Nje Tanzania; Mhe. Lim Sung-nam, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Korea Kusini; Mhe. Matilda Masuka, Balozi wa Tanzania nchini Korea Kusini; na Mhe. Salim Alharthy, Kiongozi wa Mabalozi na Balozi wa Falme ya Oman nchini Korea ya Kusini.

Monday, December 4, 2017

ASYA IDAROUS KHAMSIN KUFUNIKA SHEREHE ZA UHURU OAKLAND!


Tukiwa tunaelekea ukingoni mwa mwaka 2017 Mama wa mitindo maarufu hapa Tanzania kama Asya Idarous Khamsin, ambaye kwa sasa makazi yake ni nchini Marekani.  Ifikapo December 9th 2017  ataiwakilisha Tanzania kwa kuonyesha mitindo yake kwenye sherehe za uhuru Oakland Carlifonia.

Hivyo tukiwa kama Watanzania ni jambo la kujivunia maana Tasnia ya mitindo imekuwa ni moja kati ya vyanzo vizuri vya kuitangaza nchi yetu. Tunapaswa kuonyesha ushirikiano kwa wabunifu (Designers)  wetu wanao jituma kama Mama yetu Asya Idarous Khamsin na wengineo.

Ukiguswa unaombwa kusambaza ujumbe huu kwa Ndugu, Jamaa na Marafiki wanao penda Fashion  Asante.




Monday, September 4, 2017

NCHI SITA KUSHIRIKI MASHINDANO YA KUOGELEA YA KANDA YA TATU AFRIKA


Jumla ya nchi sita zimethibitisha kushiriki katika mashindano ya kuogelea ya kanda ya tatu ya Afrika (Cana zone 3) yaliyopangwa kufanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 19 -21.

Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya Chama Cha kuogelea nchini (TSA), Leena Kapadia amezitaja nchi hizo kuwa ni Afrika Kusini, Zambia, Kenya, Uganda, Djibouti na wenyeji Tanzania.

Kapadia amesema kuwa walitarajia kuona nchi nyingi zaidi zinashiriki katika mashindano hayo, lakini kutokana na uhaba wa fedha zimeshindwa kufanya hivyo.

“Tumezipa nafasi zaidi kutafuta fedha ili kushiriki, tutafunga mlango wa kuthibitisha wiki moja kabla ya mashindano,” alisema Kapadia.

 Alisema kuwa Tanzania itashirikisha waogeleaji 60 wakigawanywa kwa timu mbili (Tanzania A na B) chini ya makocha wao, Alex Mwaipasi na Michael Livingstone.

Nchi ambazo zimeongezewa muda wa kuthibitisha kushiriki katika mashindano ni Ethiopia, Eritrea, Somalia, Rwanda, Sudani Kusini ambazi zipo kanda ya tatu na za kanda ya nne ni Angola, Botswana, Comoro, Madagascar, Lesotho, Malawi, Mauritius, Seychelles, Msumbiji, Namibia, Zimbabwe na Swaziland.

Alisema kuwa kwa kamati yao inatafuta wadhamini kwa ajili ya kufanikisha mashindano hayo. Wanahitaji kiasi cha Sh 100 milioni ili kufanya mashindano hayo kwa hadhi inayostahili.

Alisema kuwa wanatarajia waogeleaji zaidi ya 200 kushiriki katika mashindano hayo ambayo Tanzania ni mabingwa watetezi.

Mbali ya Kapadia, kamati hiyo pia unaundwa na wajumbe ambao ni Inviolata Itatiro, Geeta Gokarn, Phillip Saliboko, Imani Dominic, Hetal, Linges Ramasamy, Thauriya Diria, Amina Karume, Nitesh Patel, Nelly Coehlo na Mary Mugurusi.

Thursday, August 31, 2017

TIMU YA JWTZ YAENDELEA KUNG'ARA KATIKA MICHEZO YA WAKUU WA MAJESHI WA AFRIKA MASHARIKI MJINI BUJUMBURA, BURUNDI


Timu ya Mpira wa kikapu  ya JWTZ  ikiimba wimbo wa Taifa kabla ya kuwafunga mabingwa wa mwaka jana Ulinzi Kenya kwa vikapu 68-58 jana mjini Bujumbura, Burundi.
Kiongozi wa safara wa timu ya JWTZ ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Michezo ya Majeshi Tanzania (BAMATA) Brigedia Jenerali Martin Amos Kemwaga akifurahia ushindi wa timu ya mpira wa kikapu jana mjini Bujumbura, Burundi.
Kiongozi wa safara wa timu ya JWTZ ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Michezo ya Majeshi Tanzania (BAMATA) Brigedia Jenerali Martin Amos Kemwaga akihojiwa na mwandishi wa ITV wa Bujumbura Bw. Balen.

Timu ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) imeendelea kung’ara katika Mashindano ya muhula wa nne wa Michezo ya Wakuu wa Majeshi wa nchi za Afrika Mashariki yanayofanyika mjini Bujumbura, Burundi. 
 Baada ya jana timu ya Mpira wa kikapu ya JWTZ kuwafunga mabingwa watetezi Ulinzi Kenya kwa vikapu 68-58, mori wa vijana wetu uliochagizwa na kauli mbiu ya HAPA KAZI TU, ulipanda tena leo katika mpira wa kikapu ambapo vijana hao hodari wa CDF Mabeyo wameibugiza Burundi kwa vikapu 94-18 bila huruma.  Na katika kabumbu pia JWTZ iliibuka kidedea kwa kuwapiga tena Warundi kwa mabao 2-1. 
“Tunashukuru Mungu kwa matokeo hayo yote”, mkuu wa msafara ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Michezo ya Majeshi Tanzania (BAMATA) Brigedia Jenerali Martin Amos Kemwaga, ameiambia Globu ya Jamii leo kwa njia ya mtandao. 
Brigedia Jenerali Kemwaga, ambaye yeye mwenyewe ni mchezaji nguli wa zamani wa mpira wa kikapu, ameeleza kufurahishwa na vijana wake ambao wamekuwa tishio katika michezo yote wanayoshiriki. 
Kaulimbiu ya Mashindano hayo ni “Shiriki michezo kama sehemu ya kazi, Kulinda Afya zetu na Kudumisha Mshikamano”, na yanahusisha nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na wenyeji Burundi. 
Timu ya JWTZ daima imekua ikifanya vizuri kwa kuchukua nafasi ya ya tatu kwa ujumla kati ya nchi zote zilizoshiriki katika mashindano yaliyofanyika hapo awali. Na safari hii timu hiyo kabambe imepania kunyakua nafasi ya kwanza kwani wao kila walipo ni HAPA KAZI TU.


Monday, August 28, 2017

JK AKIWA NCHINI INDIA KUHUDHURIA MKUTANO WA KUPAMBANA NA KUPUNGUZA VIFO VYA MAMA NA MTOTO


Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa Mkutano wa kupambana kupunguza vifo vya Mama na Mtoto, unaofanyika mjini Jaipur nchini India.
Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na baadhi ya vyombo vya habari alipokwenda kushiriki mkutano wa kupambana na kupunguza vifo vya Mama na Mtoto, unaofanyika mjini Jaipur nchini India.

WAZIRI MKUU AKUTANA NA MAKAMU WA RAIS WA CUBA


  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo ya Kikazi na Makamu wa Rais wa Cuba, Mhe. Gladys Bejarano katika mji wa Havana nchini Cuba jana August 26/2017.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo ya Kikazi na Makamu wa Rais wa Cuba, Mhe. Gladys Bejarano. katika Mji wa Havana Nchini Cuba jana August 26/2017. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

*Asisitiza nia ya kufungua ubalozi nchini humo

 WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Cuba, Mhe. Gladys Bejarano na kumuhakikishia ufunguzi wa ofisi za ubalozi wa Tanzania nchini humo.
Amesema Tanzania inayatambua na kuyathamini mahusiano mazuri ya kidiplomasia, kisiasa, kiuchumi, kielimu, kiafya na kiutamaduni kati yake na Cuba, hivyo inatarajia kufungua ubalozi nchini humo ili kurahisisha utendaji wa kazi za kibalozi.
Waziri Mkuu alikutana na Mhe.  Gladys jana jioni (Jumamosi, Agosti 26, 2017) wakati alipokuwa akihitimisha ziara yake ya kikazi nchini Cuba. Malengo ya ziara yalikuwa ni kuimarisha na kudumisha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.
“Tunatambua mahusiano mazuri yaliyopo kati Tanzania na Cuba, ambayo yalikuwepo kuanzia Serikali ya Awamu ya kwanza chini ya uongozi wa Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Nyerere, hivyo lazima tufungue ofisi za ubalozi na tutamleta balozi wetu hapa.”
Pia Waziri Mkuu ameishukuru Serikali ya Cuba kwa ujenzi wa kiwanda cha dawa za kuulia vijidudu vya maralia pamoja na ufadhili wa masomo ya udaktari inaoutoa kwa wanafunzi wa Kitanzania ambao wanasoma katika vyuo mbalimbali nchini humo.
Hata hivyo aliiomba Serikali hiyo iendelee kutoa ufadhili wa masomo kwa madaktari hao hadi ngazi ya shahada ya uzamili kwa sababu Serikali ya Tanzania inawahitaji madaktari bingwa wengi kwani walioko nchini ni wachache.
Kwa upande wake, Bi. Gladys alimshukuru Waziri Mkuu kwa kufanya ziara nchini Cuba na alimuhakikishia kwamba uhusiano wa Serikali yake na Serikali ya Tanzania utaendelea kuimarishwa kwa manufaa ya wananchi wa pande zote mbili.
Alisema Serikali ya Tanzania chini ya uongozi wa Rais Dkt. John Magufuli inafanya jitihada kubwa za kuhakikisha uchumi wake unakua kwa kasi jambo ambalo ni tofauti na mataifa mengine. “Nawapongeza kwa hatua za kimaendeleo mnazozifanya.”
Makamu huyo wa Rais alisema Serikali ya Cuba itaendelea kushirikiana na Tanzania katika uboreshaji wa Sekta za Afya, Utamaduni, Kilimo, Uchumi na Elimu. Kuhusu ombi la kuongeza ufadhili wa shahada ya uzamili kwa madaktari  alisema amelipokea na atalifanyia kazi.
Awali Balozi wa Tanzania nchini Canada, ambaye anasimamia na nchi ya Cuba, Balozi Jack Zoka alisema Serikali ya Cuba ni miongoni mwa nchi zinazoshirikiana na Tanzania katika uboreshaji wa shughuli za maedndeleo, hivyo uwepo wa ofisi za ubalozi nchini humo utazidi kuimarisha mahusiano.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU, 
JUMAPILI, AGOSTI 27, 2017.

TUNAISHUKURU SERIKALI YA CUBA KWA KUTAMBUA MASHUJAA WA AFRIKA-MAJALIWA

 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa. kushoto , akiwa na mwenyeji wake kulia ambaye ni Mkurugenzi wa Maswala ya Africa Nnchini Cuba .Balozi Jose Prieta Cintado .August 25/2017 wakiangalia Sanamu ya aliyekuwa Raisi wa Msumbiji Hayati Samora Masheli ambayo ipo katika Makumbusho ya Mashujaa wa Africa yaliopo Havana Cuba Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu .
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa .kulia pamoja na Mama Mary Majaliwa ,kushoto pamoja na mwenyeji wao katikati ambaye ni Mkurugenzi wa Maswala ya Africa Nnchini Cuba .Balozi Jose Prieta Cintado .wakiweka Shada la Maua August 25/2017 katika Makumbusho ya Mashujaa wa Africa yaliyopo Havana Cuba .Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
 
 
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameishukuru Serikali ya Cuba kwa kutambua na kuthamini mchango mkubwa uliotolewa na mashujaa wa ukombozi wa Bara la Afrika, akiwemo Baba wa Taifa Mwl. Julius Nyerere kwa kuwajengea mnara wa kumbukumbu.

Mnara huo umejengwa katika Manispaa ya Playa jijini Havana kwenye eneo maalumu la makumbusho ya mashujaa hao walioshiriki katika ukombozi wa Afrika, ambapo zimewekwa sanamu zao pamoja na maelezo mafupi ya historia zao na nchi wanazotoka.

Waziri Mkuu alifanya ziara katika eneo hilo jana (Ijumaa, Agosti 25, 2017) na  kuweka shada la maua katika mnara huo uliozungukwa na sanamu za mashajuaa wa Bara la Afrika na kuoneshwa sehemu itakayowekwa sanamu ya Mwl. Nyerere.

Akiwa katika eneo hilo, Waziri Mkuu aliishukuru Serikali ya Cuba kwa kujenga makumbusho ya mashujaa hao na kwamba Serikali ya Tanzania itashirikiana na Cuba kuhakikisha kuwa sanamu ya Mwl. Nyerere inawekwa katika sehemu iliyotengwa.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Instuto Cubano De Amistad Con El Pueblo (Taasisi ya Ushirikiano wa Cuba na Nchi Marafiki), Bw. Jose’ Prieto Cintado alisema mnara huo umejengwa kwa lengo la kutambua thamani na umuhimu wa viongozi hao.

Mkurugenzi huyo alisema Serikali ya Cuba inathamini mchango mkubwa uliotolewa na mashujaa hao katika vita ya ukombozi wa Bara la Afrika, ambapo iliamua kujenga mnara wa kumbukumbu katika nchi yao.

Alisema wananchi wa Cuba pamoja na watu kutoka mataifa mbalimbali ndani na nje ya Bara la Afrika wanakwenda katika eneo hilo la makumbusho na kujifunza historia za viongozi hao. Pia eneo hilo linatumiwa na watafiti wa masuala ya kihistoria.

Mashujaa ambao tayari sanamu zao zimekwishawekwa kwenye eneo la kuzunguka mnara huo ni pamoja na Jomo Kenyatta (Rais wa kwanza wa Kenya), Modibo Keita (Rais wa Mali), Amilcar Cabral (Rais wa kwanza wa Guinea Bissau).

Wengine ni Dkt. Kwame Nkrumah (Rais wa kwanza Ghana), Oliver Thambo (Kiongozi Mwandamizi wa Chama cha Ukombozi cha ANC cha Afrika Kusini), Eduardo Chivambo Mondlane (Kiongozi wa ukombozi nchini Msumbuji).

Wengine ni Samora Moises Machel (Rais wa kwanza wa Msumbuji), Sekou Toure (Rais wa kwanza wa Senegal), Seretse Khama (Rais wa kwanza wa Botswana), Alhaji Aboubakar Tafawa Balewa na Obafemi Jeremiah Awolowo (Mawaziri Wakuu wa zamani wa Nigeria) na Chifu Jeremia Azikiwe (Rais wa zamani wa Nigeria) .
 

Saturday, August 26, 2017

UKAID NA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO YAZINDUA PROGRAM YA MAFUNZO KWA WATUMISHI


Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), na viongozi waandamizi wa UKAID-DFID, British Council-Tanzania, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako, na watumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango walionufaika na ufadhili huo (kushoto) wakifurahia baada ya kuzinduliwa rasmi kwa mpango wa miaka mitano wa ufadhili wa masomo kwa ngazi ya shahada ya uzamili katika vyuo vikuu vya nchini Uingereza katika Nyanja za uchumi, mipango, usimamizi wa fedha za umma na sheria za kimataifa uliotolewa na Serikali ya Uingereza kwa Wizara hiyo.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa tatu kulia), Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Uingereza (UKAID-DFID), Bi. Beth Arthy (wa tatu kushoto), Mkurugenzi Mkazi wa British Council, Bi. Angela Hennelly na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (Mb) (wa pili kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa Serikali na Watumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango waliopata ufadhili wa Mafunzo kutoka UKAID-DFID, muda mfupi baada ya kuzindua rasmi program hiyo, Jijini Dar es Salaam. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha na Mipango)​
Wafanyakazi watano wa Wizara ya Fedha na Mipango (Walioketi) waliopatiwa udhamini wa masomo nchini katika vyuo vikuu nchini Uingereza kwa kiwango cha Shahada ya Uzamili uliotolewa na Shirika la Maendeleo la Uingereza (UKAID-DFID), wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa British Council-Tanzania ambao ndio waratibu wa Program hiyo ya miaka mitano, itakayogharimu Shilingi bilioni 3.6 kwa  lengo la kuongeza ujuzi na umahili wa rasilimali watu katika masuala ya uchumi, mipango, usimamizi wa fedha za Umma na Sheria za kimataifa. Kutoka kushoto Harieth Lubinga, John Kabiti, Susan Mbayuwayu, Peter Kalugwisha na Gloria Mduda.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia) akiongea ofisini kwake na Mkurugenzi Mkazi wa Idara ya Kimataifa ya Maendeleo kutoka Serikali ya Uingereza (UKAID-DFID), Bi. Beth Arthy, kuhusu masuala mbalimbali ukiwemo ufadhili wa miaka mitano wa Taasisi hiyo wa masomo ya juu nchini Uingereza kwa wafanyakazi wa Wizara hiyo katika ngazi ya Shahada ya Uzamili.

WAZIRI MKUU ATEMBELEA KIWANDA CHA KUZALISHA SUKARI NCHINI CUBA


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipata maelezo ya ukarabati wa kiwanda cha Sukari cha UGB  kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari nchini Cuba Bwana Francisco Martin, jana August 24/2017 kiwanda hicho kipo katika Mji wa San Nicola's de Bari nchini Cuba
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiangalia shehena ya sukari iliyozalishwa katika kiwanda cha UGB Central Azucarero 30 Noviembre wakati alipotembelea kiwanda hicho jana August 24/2017 kilichopo katika mji wa San Nicola's de Bari nchini Cuba.

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Shirika la Viwanda vya Sukari nchini Cuba, Bw. Francisco Lled, ambaye amekubali kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kuongeza uzalishaji wa sukari nchini.

Shirika la Sukari la nchini Cuba linauwezo wa kuzalisha tani milioni nne za sukati kwa mwaka huku mahitaji ya ndani ni tani 700,000, ambapo kiasi kinachobaki huuzwa nje ya nchi. Kwa sasa shirika hilo linazalisha tani milioni mbili tu katika viwanda vyake 56.

Waziri Mkuu alikutana na Bw. Lled jana (Alhamisi, Agosti 24, 2017), wakati alipofanya ziara katika kiwanda cha kuzalisha sukari cha UGB Central Azucarero 30 de Noviembre katika mji wa San Nicola’s de Bari ambacho ni kati ya viwanda 27 vya shirika hilo linalomilikiwa na Serikali ya Cuba kwa asilimia 100.

Katika mazungumzo yao Waziri Mkuu alimshawishi Bw. Lled kuja nchini kwa ajili ya kuwekeza katika ujenzi wa viwanda vya kuzalisha sukari. Alisema kwa sasa Tanzania kuna viwanda vikubwa vitano vya sukari ambavyo uzalishaji wake hautoshelezi mahitaji ya ndani.

Waziri Mkuu alivitaja viwanda hivyo ambavyo ni Mtibwa na Kilombero (Morogoro), Mahonda (Zanzibar), TPC (Kilimanjaro) na Kagera ambavyo vyote vinazalisha jumla ya tani 320,000 za sukari kwa mwaka huku mahitaji yakiwa ni zaidi ya tani 400,000.

Hata hivyo, Waziri Mkuu alisema Serikali kwa kushirikiana na sekta binafsi inatarajia kujenga viwanda vitatu vya kuzalisha sukari, ambavyo vitazalisha sukari itakayotosheleza mahitaji na ndani ya nchi na kiasi kitakachosalia kitauzwa nje.

Tuesday, August 22, 2017

JACK PEMBA ALIPIA HOTEL WACHEZAJI WA SIMBA NA ANATAFUTA UWEZEKANO WACHEZAJI WA SIMBA WASHUKE NA CHOPA UWANJANI



Uwanja wa mpira wa kikapu Bonanza ltakapopigiwa address 
6615 Dublin center Dr,
Dublin, OH 43017

Uwanja utakaopigiwa mechi ya watani wa jadi Simba na Yanga address
Columbus Global Academy Stadium, 
4077 Karl rd, 
Columbus, OH 43224

Jack Pemba mfanyabishashara mweye pesa ndefu ambaye kwa sasa anaishi umangani na ambaye atakuwepo kwenye mtanange wa Simba na Yanga Columbus, Ohio amewachukulia wachezaji wa Simba vyumba kwa kukuaa watakapokua Columbus, Ohio wakati wa mechi yao na Yanga inayosubiliwa kwa wingi na wadau wa Columbus, na vitongoji vya jirani.

Boss Jack Pemba pia alikua akiangalia uwezakano wa kuwaleta wachezaji wa Simba kwenye mtanange huo kwa kuwakodishia chopa.

Mechi hiyo ya watani wa jadi inatarajiwa kuchezewa kwenye stadium ya Global Academy iliyopo Columbus na itachezwa baada ya bonanza la mpira wa kikapu.

WAZIRI MKUU MAJALIWA AKUTANA NA WANATANZANIA WAISHIO NCHINI CUBA


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (katikati) akizungumza na wanafunzi wanaosomea fani ya Udaktari nchini Cuba, alipokutana nao katika Hotel ya Nacional de Cuba, jana Agosti 20, 2017. kushoto ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanafunzi Cuba, Goodchance Tarimo na kulia ni Ofisa wa Ubalozi wa Tanzania Nchini Canada na Cuba, Leonce Bilauri. Waziri Mkuu yupo Havana Cuba kwa Ziara ya Kikazi
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (kulia) akisalimiana na wanafunzi wa Kitanzania anaye Soma fani ya Udaktari nchini Cuba, Eshe Hemed Rashid pamoja na Nasra Sheikhan, alipokutana nao katika Hoteli ya Nacional de Cuba, jana Agosti 20, 2017
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi Wakitanzania wanao someafani ya Udaktari nchini Cuba.

Wednesday, August 16, 2017

MAHOJIANO NA MCH ABSALOM NASUWA KUHUSU MKUTANO WA ASKOFU GWAJIMA DC

Karibu na asante kwa kujiunga nasi
Kanisa la Umoja International Outreach lililopo jijini Dallas Texas limeandaa mikutano ya injili katika maeneo ya Texas na Washington DNV.
Mwanzilishi na Mchungaji kiongozi wa kanisa hilo, Mch Absalom Nasuwa alizungumza nami kuhusu mkutano huo
KARIBU

Pia Mch Nasuwa alizungumzia huduma yake

Tuesday, August 15, 2017

KONGAMANO LA NNE LA KITAIFA LA WATANZANIA WANAOISHI NJE (DIASPORA) KUFANYIKA TAREHE 23 NA 24 AGOSTI

 Katibu Mkuu Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Salum Maulid Salum, akitoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya kongamano la nne la kitaifa la Watanzania wanaoishi nje litakalofanyika tarehe 23 na 24 Agosti hapa Zanzibar. Hafla hiyo imefanyika Ikulu mjini Zanzibar.

 Katibu Mkuu Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Salum Maulid Salum, akitoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya kongamano la nne la kitaifa la Watanzania wanaoishi nje litakalofanyika tarehe 23 na 24 Agosti hapa Zanzibar. Hafla hiyo imefanyika Ikulu mjini Zanzibar.

  Mkurugenzi wa PPR Pascal Mayalla akiuliza suali katika mkutano na waandishi wa habari uliozungumzia Kongamano la kitaifa la Watanzania wanaoishi nje uliofanyika Ikulu mjini Zanzibar.
Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa na Uratibu wa Wazanzibari wanaoishi nje ya nchi Bi. Adila Hilali Vuai akijibu masuali yaliyoulizwa na wandishi wa habari kuhusu maandalizi ya kongamano la kitafa litalofanyika tarehe 23 na 24 Agosti hapa Zanzibar. (kushoto) Muandishi wa habari Rahma Suleiman wa Chuchu Fm Redio.
Picha na Makame Mshenga.

Tuesday, August 8, 2017

VIJANA KUTOKA MJI WA VALLEJO, CALIFORNIA WATEMBELEA UBALOZI WETU WASHINGTON D.C.

Vijana sita wa Kimarekani kutoka Mji wa Vallejo, California,  (Sister City International) leo  wametembelea Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani jijini  Washington D.C. Mji wa Vallejo ni Mji Dada na Mji wa Bagamoyo. Lengo la ziara yao ni  kujua na kujifunza masuala mbalimbali kuhusu Tanzania, kwa kuwa wanatarajia kutembelea mji wa Bagamoyo mwaka 2019.


Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Wilson M. Masilingi (kati) na afisa wa ubalozi Bw. Dismas Assenga (kulia) wakiwa na vijana  hao sita kutoka mji wa Vallejo, California

ROSE MMBAGA ASHINDA TUZO YA MWANAMKE MWENYE USHAWISHI



Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Msichana wa kitanzania, Rose Mmbaga ameweza kushinda tuzo ya Mwanamke mwenye Ushawishi ‘Women in Events Hall of Fame’ ya nchini Marekani na kuwa ni Mwafrika pekee katika kusaidia vijana katika maswala ya masuala ya Mazingira.

Mmbaga ameshinda tuzo hiyo kutokana na uwezo wake wa ushawishi katika kazi za kijamii ambazo amezifanya nchi nzima.

Amesema kuwa Safari yake ilianza na kujitolea kwa takribani miaka mitatu baada ya kuona ajira zinasumbua, na alianza na VSO international kwenye mradi wa International Citizen Service alafu nikajiunga na Restless development katika mradi wa kijana tung’are kazini chini ya International Citizen Service programu kwa takribani miezi sita na tena nikaenda Raleigh Tanzania kwenye mradi wa Expedition.

“nilijenga shule kusaidia watoto yatima,mashirika yote nilishirikiana na vijana kutoka ndani na nje ya nchi na miradi ilifadhiliwa na DFID yani serikali ya wingereza.Haikua rahisi lakini leo hii naweza kuona matunda ya kujitolea katika jamii yangu.”amesema Rose.

Kupitia safari yangu leo hii nimeweza kupata tuzo ya kimataifa kutoka Association for women in events,Hall of fame kama “Woman of Influence”(Mwanamke mwenye ushawishi) ambayo walioniwezesha ni watu ambao wanafahamu kazi yangu na nilioshirikiana nao katika kazi zangu haswa vijana wa kitanzania na wengi wao ni wale waliojitolea

Amesema pongezi zinamwendea mwanaharakati wa kuwasaidia wanawake duniani Mandy Sanghera ameweza kuwa wa kwanza kuninominate jina langu kati ya wanawake wengi na leo hii ninamshukuru kwa kupitia yeye nimeweza kushinda.

Monday, August 7, 2017

NDUGAI AMTEMBELEA NA KUFANYA MAZUNGUMZO RAIS WA IRAN


Mheshimiwa Spika Job Ndugai leo amemtembelea Ikulu na kufanya mazungumzo na Rais wa Iran alieapishwa jana,Mhe Hassan Rouhani ambapo Mheshimiwa Spika amempongeza kuteuliwa kwake kwa mara ya pili na kumuahidi ushirikiano wa karibu baina ya Bunge la Tanzania na la Iran. Mheshimiwa Spika alikuwa ni miongoni mwa wageni mashuhuri walioalikwa kushuhudia kuapishwa kwa Rais Rouhani katika sherehe zilizofanyika kwenye Bunge la Iran mjini Tehran.

Friday, August 4, 2017

MKUTANO MKUU WA UCHAGUZI WA JUMUIYA YA WATANZANIA NORTHAMPTON, UINGEREZA, KUFANYIKA JUMAMOSI AGOSTI 19, 2017



Ndugu wana Northampton kwa mujibu wa taratibu na kanuni tulizojiwekea na matarajio yetu ya muda mrefu, Kwa niaba ya kamati ndogo ya maandalizi naitisha Mkutano Mkuu na wa Uchaguzi wa Viongozi Wapya wa Jumuiya yetu ya Watanzania wote waishio Northampton na maeneo ya Wellingborough, Kattering na Corby (NORTHAMPTONSHIRE)  utakaofanyika siku ya Jumamosi tarehe 19/08/2017 katika ukumbi wa Norfolk Terrace, Semilong, Northampton NN2 6HS - Kuanzia saa kumi kamili jioni (4pm) mpaka saa mbili usiku (8.00pm).


Kamati ya maandalizi  inaomba ushirikiano wenu ili Kuepuka kupoteza muda siku ya mkutano, Tunaomba kila mjumbe mwenye ajenda ya ziada yeyote ambayo angependa iwepo katika kikao chetu basi asisite kunipatia siku nne kabla ya mkutano kwa njia ya Barua Pepe kwenda; suleimansalum160@yahoo.com au kwa kupiga simu ya Mkononi nambari 07963549935.
Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Mwenyekiti wa  Tanzania Diaspora Community/Association in the United Kingdom of Great Britain and Northern Ireland Ndugu Abraham Sangiwa, ambaye atatoa ufafanuzi wa jinsi Jumuiya zetu hapa Northampton zitakavoshirikiana na Jumuiya hii kuu katika malengo muhimu yanayotugusa wote Kama Watanzania tunaoishi Ughaibuni ili kupata ufumbuzi wenye nguvu zaidi kwa ushirikiano wetu.



Tujitahidi kuzingatia muda siku hiyo.  
UMOJA NA NGUVU
Suleiman Salum
Mwenyekiti Jumuiya ya Watanzania Northampton

Thursday, August 3, 2017

WASHIRIKI KUTOKA TANZANIA WA “YOUNG AFRICAN LEADERS INITIATIVE (YALI) 2017” WATEMBELEA UBALOZI WA TANZANIA, WASHINGTON, D.C


Balozi Tanzania nchini Marekani, Wilson M. Masilingi akizungumza na Washiriki wa YALI, Mandela Wahington Fellows. (kulia) Afisa wa Ubalozi, Dismas Assenga.
Yali Mandela Washington Fellows 2017 wakiongea na Mhe. Balozi.
Balozi Wilson M. Masilingi akiwa na washiriki wa YALI Mandela Washington Fellows, 2017.

Tarehe 2, Agosti 2017) Washiriki 42 wa Mandela Washington Fellowship 2017 kutoka Tanzania waliofika mwezi Juni, 2017, walitembelea Ubalozi wa Tanzania, Washington, D.C. na kukutana na Balozi Wilson M. Masilingi. 

YALI, ni programu iliyoanzishwa na Rais mstaafu wa Marekani, Barack Obama kuwasaidia vijana wa Afrika kutembelea Vyuo vikuu vya Marekani kujifunza, kwa ufadhili wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani (U.S. Department of State). Baada ya kumaliza mafunzo katika vyuo mbalimbali Watanzania hao walitembelea Washington, D.C. kupokea vyeti na kutembelea Ubalozi wa Tanzania.

Balozi Masilingi aliwaasa kuwa wazalendo, kupendana na kuwa waadilifu katika kuendeleza uchumi wa nchi yetu kwa kuanzisha na kukuza biashara. Aliwashauri pia kushirikiana na Ubalozi na Diaspora ya Watanzania waliopo Marekani, kukuza sekta ya utalii, biashara, elimu na ujenzi wa viwanda.

MAMA WA MITINDO KUONYESHA MAVAZI YAKE JUKWAANI USA 4-5/8/2017

 
 Inawezekana kuna watu ambao hawajui umuhimu wa Fashion, kumbuka Fashion ni kitu muhimu sana kwa sababu bila Fashion tusinge weza kwenda na wakati kimavazi, hivyo tunapaswa kuwapongeza sana wanamitindo ambao wanaendelea kutuletea mitindi mipya na mizuri ya mavazi Tanzania.
Sasa basi kwa umahiri wake Mma wa mitindo, ambaye ni mkombozi wa Designers wengi hapa Tanznaia, Designer maarufu kama Asya Khamsin Kesho Ijumaa na Jumamosi 5/8/2017 atakuwa kwenye jukwaa akionyesha mitindo yake Washington DC USA, katika tukio la Kenya Reunion mjini Maryland.
Kwako mdau wa mitindo na Fashion, huu ni wakati wako kuendelea  kuonyesha upendo kwenye Tasniya ya hii ili tuzidi kutambulika kimataifa zaidi na mavazi yetu ya Africa